Sisi tukiwa kituo rasilimali cha kimataifa kujibu maswali yako yote yanayohusu matumizi ya vidonge vya kutoa mimba. Kila nchi ina kanuni, sheria na dhana zake kuhusu utoaji mimba. Lengo letu ni kuondoa taarifa potofu na kueleza ukweli kuhusu matumizi ya vidonge vya kutoa mimba – cha kufikiria kwanza, ni wapi zinapatikana, kufanya matumizi salama, matarajio yakuwa nayo na wapi pa kupata msaada wa kitabibu.

Dawa mbili zinazotumika zaidi kwa ajili ya kutoa mimba ni Mifepristone na Misoprostol. Tunaelezea njia zote mbili (mchanganyiko wa Mifepristone na Misoprostol, na Misoprostol peke yake) ikiwa ni pamoja na jinsi ya kumeza vidonge ili uweze kutoa mimba kwa usalama.

Orodha ya Vitu vya Kuangalia:

Matayarisho kabla ya kumeza vidonge

  • Vitambaa vya wanawake (Pedi)
  • Maji ya kunywa ya kutosha
  • Chakula laini chenye lishe
  • Dawa ya maumivu ya Ibuprofen au dawa nyingine za maumivu
  • Namba ya simu ya mtaalamu wa afya na mpango maalum kama dharura itatokea
  • Rafiki wa karibu au ndugu wa karibu wa kukusaidia