Dhamira:

Dhamira yetu ni kuhudumia kama kituo cha rasilimali cha kimataifa cha kujibu maswali yote kuhusu matumizi ya vidonge vya kutoa mimba. Leo hii, kila nchi ina sheria na maoni yake ya kitamaduni kuhusu utoaji mimba. Lengo letu ni kuondoa taarifa potofu na kueleza ukweli kuhusu matumizi ya vidonge va kutoa mimba ili mahali popote utakapokuwa uweze kufahamu matumizi salama ya vidonge hivi.

Tovuti hii ilianzishwa na inaendeshwa na kundi la watu wenye ari ambao wanaamini kuwa kila mwanamke aweze kupata huduma ya utoaji wa mimba salama. Taarifa za tovuti hii zilikusanywa kutoka kwenye vyanzo vinavyoaminika ikiwa ni pamoja na Shirika la Afya Duniani, Taasisi ya Guttmacher na safe2choose.org, kuhakikisha kwamba taarifa zinazoenda na wakati kuhusu vidonge vya utoaji mimba zinapatikana kwa urahisi kwa ajili ya usalama na afya ya wanawake wote.

Katao

Kila jitihada inafanyika kuhakikisha taarifa zilizomo kwenye kurasa za tovuti hii ni sahihi. Hata hivyo maelezo yanaweza kubadilika mara kwa mara na waandishi hawatakubali dhima kwa ajili ya uhakika wa taarifa zinazotolewa wakati wowote.