Maelekezo ya matumizi ya Mifepristone NA Misoprostol

Hatua ya 1: Meza kidonge kimoja cha mifepristone (Mikrogram 200), unaweza kutokwa damu kidogo baada ya kumeza mifepristone. Hii ni kawaida!

Hatua ya 2: Subiri kati ya masaa 24 – 48

Lazima usubiri kwa muda wa masaa 24 kabla ya kutumia misoprostol, lakini hakikisha unatumia kabla ya masaa 48. Wakati unasubiri, endelea kufanya shughuli zako za kawaida unazofanya kila siku kama vile kuangalia watoto au kwenda kazini au shule.

Hatua ya 3: Tumia misprostol (vidonge 4 vyenye Mikrogram 200 kila kimoja)

Kuna njia mbili za kutumia misoprostol: Kuweka vidonge kwenye uke wako au mdomoni katikati ya mashavu na taya la chini. Njia zote mbili zina ufanisi mkubwa:

vaginaKama unatumia njia ya kuweka misoprostol ndani ya uke wako

 1. Osha mikono yako kwa maji na sabuni.
 2. Lala chini na kwa kutumia kidole sukuma vidonge vine (4) ndani ya uke. Sio lazima vidonge viwe kwenye sehemu maalumu ndani ya uke, ingiza mpaka pale tu kidole chako kinapofikia.
 3. Lala chini wa muda wa dakika 30.

mouthIkiwa unatumia njia ya kuweka misoprostol mdomoni

 1. Kunywa maji ili kufanya midomo yako kuwa minyevu. Weka vidonge vinne katikati ya mashavu na meno ya chini au fizi (kila shavu vidonge viwili)
 2. Tulia bila kutafuna kwa dakika 30. Wakati dawa inayeyuka inaweza kufanya mdomo wako kukauka au kupata ladha ya chaki. Usile wala kunywa chochote kwa kipindi hicho cha dakika 30.
 3. Baada ya dakika 30, sukutua mdomo wako na maji na meza dawa yote iliyobaki mdomoni.


Nini kinafuata?

Kwa kawaida ndani ya saa moja hadi mawili, utaanza kupata maumivu ya tumbo na kutokwa na damu. Kunywa maji na kula chakula jinsi utakavyoweza, lakini uwe na mpango wa kukaa sehemu tulivu, mahali pa faragha mpaka utakapojisikia vizuri. Wanawake wengi hujisikia vizuri chini ya masaa 24. Dawa ya Ibuprofen ni dawa nzuri kupunguza maumivu. Unaweza kununua Ibuprofen ya milligram 200 bila ya karatasi ya dawa kutoka kwa daktari kwenye nchi nyingi.

Kwa maelezo zaidi, soma ukurasa wa “Maudhi madogo madogo

Hatua ya 4:

Kama umetumia vidonge vya kutoa mimba vya mifepristone na misoprostol, huenda usihitaji kwenda kwa mtoa huduma ya afya kwa ajili ya uchunguzi. Hakikisha huna dalili zozote za ujauzito, uwe unajisikia mwenye afya nzuri na damu inayotoka sio nyingi. Dawa hizi zina ufanisi mkubwa na Shirika la Afya Duniani (WHO); linapendekeza kuwa upate huduma ya matibabu pale utapojisikia hali zifuatazo:

 • Kuumwa au kama maumivu hayapungui. Usisubiri mpaka wiki mbili kama una matatizo haya; Tafuta msaada wa kitabibu haraka.
 • Kama bado unahisi dalili za ujauzito wiki 2 baada ya kutumia dawa ya kutoa mimba.
 • Unatoka damu nyingi na haipungui hata baada ya wiki mbili.

Angalizo: Wiki mbili baada ya kutoa mimba, vipimo vitaendelea kuonyesha kua bado una ujauzito hii inatokana na homoni zilizoko ndani ya mwili wako. Kama bado unahisi dalili za ujauzito (maumivu ya matiti, kichefuchefu, uchovu n.k) baada ya kutumia vidonge, muone daktari.

Maelekezo – Misoprostol Peke Yake

Maelekezo haya ni kama unatumia vidonge 12 vya misoprostol vya Mikrogram 200 kila kimoja. Kuna njia mbili za matumizi ya misoprostol: Kuweka vidonge kwenye uke wako au mdomoni katikati ya mashavu yako na taya la chini. Njia zote mbili zina ufanisi mkubwa.

Hatua ya 1aTumia vidonge 4 vya kwanza

 • vaginaKama unachagua kuweka vidonge kwenye uke wako, hakikisha unakojoa kwanza na unaosha mikono yako kwa maji na sabuni. Lala chini na tumia kidole kusukuma vidonge vinne ndani ya uke wako. Sio lazima vidonge viwe kwenye sehemu maalumu ndani ya uke, ingiza mpaka pale tu kidole chako kinapofikia. Lala chini kwa dakika 30 zinazofuata.

 

 • mouthKama unachagua kuweka vidonge mdomoni, weka vidonge katikati ya mashavu yako na meno ya chini au fizi (kila shavu vidonge viwili), tulia bila kutafuna kwa dakika 30. Wakati dawa inayeyuka mdomoni kwako inaweza kusababisha mdomo kukauka au kupata ladha ya chaki. Usile wala kunywa chochote kwa kipindi hicho cha dakika 30. Baada ya muda kwisha, sukutua mdomo wako na maji na meza dawa yote iliyobaki mdomoni.

1b: Subiri masaa 3 mpaka 4 kabla hujaendelea na hatua ya 2.

Hatua 2a: Kumia vidonge 4 ya ziada, rudia hatua ya kwanza. Kama umechagua njia ya kuweka vidonge ukeni, lala chini au fizi kwa dakika 30, au kama unatumia njia ya kuweka mdomoni, weka vidonge katikati ya mashavu na meno ya chini na shikilia kwa dakika 30 kabla ya kuvimeza kwa kutumia maji.

2b: Subiri masaa 3 mpaka 4 kabla hujaendelea na hatua ya 3.

Hatua ya 3: Kutumia vidonge 4 vya mwisho, rudia hatua ya kwanza.  Kama umechagua njia ya kuweka vidonge ukeni, lala chini kwa dakika 30, au kama unatumia njia ya kuweka mdomoni, weka vidonge katikati ya mashavu na meno ya chini na hakikisha unasubiria kwa dakika 30 kabla ya kuvimeza kwa kutumia maji.


Nini kinafuata?

Kwa kawaida ndani ya saa 1 hadi 2 baada ya vidonge vya kwanza kuyeyuka na kuingia mwilini mwako, utaanza kupata maumivu na kutokwa na damu. Kunywa maji na kula chakula jinsi utakavyoweza, lakini uwe na mpango wa kukaa sehemu tulivu, mahali pa faragha mpaka utakapojisikia vizuri. Unaweza kunywa dawa ya maumivu ya ibuprofen au dawa nyingine za kutuliza maumivu zinazopatikana madukani. Wanawake wengi hujisikia vizuri chini ya masaa 24.

Kwa maelezo zaidi, soma ukurasa wa “Maudhi madogo madogo

Hatua ya 4: Onana na mtoa huduma wa afya

Kama umetumia misoprostol peke yake, ni vizuri kufanyiwa uchunguzi na mkunga, nesi au daktari ndani ya wiki 2 mpaka 3 baada ya kutumia vidonge. Kwa kufanya kipimo cha kizazi, wahudumu wa afya kugundua kama bado ni mjamzito. Kama hutaki kufanya kipimo cha kizazi, unaweza kufanyiwa kipimo cha ultrasound (kama inapatikana). Kama unaweza, tunakuhimiza kumwambia mtoa huduma wa afya kwamba umetumia vidonge vya utoaji mimba. Kama ukihisi si salama kumshirikisha mtoa huduma wa afya, au kama utoaji mimba hauruhusiwi hapo ulipo, unaweza kuwaambia kwamba unafikiri ulikuwa na ujauzito na kisha ukaanza kutokwa na damu au unaweza kusema umekuwa ukitokwa na ambayo inaonekana kidogo tofauti na hedhi yako ya kawaida.

Lazima kumuona mhudumu wa afya kama unajisikia:

 • Kuumwa au maumivu hayapungui. Usisubiri mpaka wiki mbili kama una matatizo haya, pata msaada wa kitabibu haraka.
 • Unatoka damu nyingi na haipungui hata baada ya wiki mbili.
 • Kama bado unahisi dalili za ujauzito wiki 2 baada ya kutumia dawa ya kutoa mimba.

Angalizo: Wiki mbili baada ya kutoa mimba, vipimo vitaendelea kuonyesha kua bado una ujauzito hii inatokana na  homoni zilizoko ndani ya mwili wako. Kama bado unahisi dalili za ujauzito (maumivu ya matiti, kichefuchefu, uchovu n.k) baada ya kutumia vidonge, muone daktari.