Utajisikiaje baada ya kutumia vidonge vya kutoa mimba?

Maumivu ya tumbo na kutokwa damu ndio matokeo makubwa. Dalili hizi ni nzuri kwa sababu inaonyesha kuwa dawa inafanya kazi. Lakini, ni kwa kiasi gani utapata maumivu ya tumbo na kutokwa na damu?

  • Kwa wanawake wengine, maumivu ya tumbo ni makali sana – zaidi kuliko maumivu wakati wa hedhi (kama unapata maumivu ya tumbo wakati wa hedhi).
  • Kwa wanawake wengine, hutokwa na damu nyingi kuliko inayotoka wakati wa hedhi. Unaweza kutoka mabonge ya damu ya ukubwa wa yai la kuku ndani ya masaa machache baada ya kunywa misoprostol.
  • Kwa wanawake wengine, maumivu ni kidogo na damu inayotoka sawa na ile ya wakati wa hedhi.

 

 

Tunataka uwe tayari!:

  • Usishtuke ukitokwa na damu zaidi kuliko hedhi ya kawaida. Hii ni kawaida.
  • Ukipata maumivu ya tumbo, dawa ya Ibuprofen ni dawa nzuri kupunguza maumivu. Unaweza kununua Ibuprofen ya milligram 200 bila ya karatasi ya dawa kutoka kwa daktari kwenye nchi nyingi. Kunywa vidonge 3-4 kila baada ya masaa 6-8. Hii itakusaidia kupunguza maumivu ya tumbo.

 

Kuwa Mwangalivu

Wakati mimba inavyotoka, dalili hap juu ni kawaida. Kuwa makini. Chini ni baadhi ya ishara kwamba unaweza kuwa katika hatari ya kupata matatizo makumbwa.bleeding image

Kiwango cha utokaji damu:
Kama utaloanisha pedi mbili kubwa kwa masaa mawili mfululizo baada ya mimba kutoka, huku ni kutokwa na damu nyingi sana. Unatakiwa kupata msaada wa kitabibu kama unatoka damu nyingi kiasi hiki. Kuloanisha pedi inamaanisha pedi kubwa yote imeloana damu mbele na nyuma, pembeni na pembeni na juu mpaka chini.

Maumivu Makali: Kama unapata maumivu makali sana ambayo hayapungui hata baada ya kunywa dawa ya Ibuprofen, pata msaada wa kitabibu. Maumivu makali sana huenda ikamaanisha umepata matatizo makubwa ya mimba. Maumivu yasiyopungua ambayo hayapungui hata baada ya kunywa dawa ya Ibuprofen inaweza kuwa dalili ya hatari. Tunashauri mwanamke yeyote mwenye mimba nayepata maumivu atafute msaada wa kitabibu.

Unajisikia kuumwa sana?: Unaweza kupata homa, kichefuchefu na kutapika siku ambayo umekunywa misoprostol ambayo ni kitu cha kawaida. Unatakiwa kujisikia nafuu zaidi kila siku baada ya kutumia vidonge vya kutoa mimba, na sio kuumwa. Kama utajisikia kuumwa Zaidi siku yoyote baada ya kumeza misoprostol unahitaji msaada wa kitabibu haraka.