• Kama unahitaji kutunza siri na kufanya utoaji mimba wako wa faragha jinsi inavyowezekana, tumia vidonge vya utoaji mimba kwenye pande za mdomo katikati ya mashavu na meno ya chini. Katika hali isiyo ya kawaida ukipata tatizo kubwa na kulazimika kupata msaada wa kitatibabu, mabaki ya vidonge yanaweza kuonekana ukeni. Kwenye nchi nyingine, taarifa inaweza kutolewa kuwa mabaki ya dawa yameonekana kwenye uke wako.
 • Ujauzito wako ni wa muda gani? Utafiti unaonyesha kuwa mara nyingi utoaji mimba kwa kutumia vidonge unapendekezwa kwa mimba zenye umri chini ya wiki 10. Tumia kikokotoleo (calculator) hiki kujua ujauzito una muda gani?
  Kama siku ya kwanza ya hedhi iliyopita ilianza tarehe au baada ya tarehe:
  April 18th, 2017
  bado unaweza ukatumia vidonge vya kutoa mimba.
 • Nani unayemtegemea kama unahitaji msaada wakati wa kutoa mimba? Nani unamwamini kama utahitaji msaada wa kitatibabu? Kwenye nchi nyingine kuna sheria kali za kiutamaduni na kijamii kuhusu utoaji mimba. Ni vizuri kuwa na taarifa hizi ili matatizo yatatokea ujue ni nani wakunamtegemea kukupa msaada.

Kabla ya kunywa vidonge

 • Kama umeweka kitanzi/lupu kwenye kizazi chako (kwa mfano coil au yenye homni ya progesterone) lazima kiondolewe.
 • Kama unanyonyesha mtoto, dawa ya misoprostol inaweza kusababisha mtoto kuhara. Ili kuepuka hili, mnyonyeshe mtoto kwanza ndipo unywe dawa ya misoprostol halafu subiri masaa 4 kabla ya kumnyonyesha tena mtoto.
 • Kama wewe unaishi na maambukizi ya Virusi Vya UKIMWI (VVU), hakikisha huumwi zaidi, unatumia dawa za kupunguza makali ya VVU na afya yako ni nzuri.
 • Kama una upungufu wa damu, itakuwa ni vyema kumfahamu mtoa huduma ya afya ambaye anaweza kukusaidia kama utahitaji msaada. Kama una upungufu mkubwa wa damu (upungufu wa madini ya chuma kwenye damu yako) na unatumia vidonge vya kutoa mimba ikafanya utokwe damu nyingi, afya yako inaweza kuwa hatarini.

Ushauri wa Jumla

 • Kunywa maji mengi kipindi chote cha mchakato huu
 • Kula chakula kidogo (kwa mfano vyakula vikavu au vya kukausha inaweza kukusaidia usipate kichefuchefu)
 • Wakati wa kunywa vidonge vya misoprostol, kuwa katika maeneo (kama nyumbani) ambapo utapata faragha na kuweza kulala kwa masaa kadhaa baada ya kunywa dawa.
 • UKuwa na mtu mmoja ambaye ataweza kukupatia kama chai ya moto au kitu cha chakula na kukuangalia kama unapenda, inaweza ikasaidia.
 • Hakikisha una vitambaa vya wnawake (pedi) za kutosha. Kuna uwezekano ukatumia nyingi zaidi kuliko kwenye hedhi ya kawaida.
 • Uwe umepanga kituo cha afya utakachopelekwa kama utahitaji matibabu zaidi.