Jinsi ya kujiandaa kwa ajili ya kutoa mimba

Ni muhimu kupata taarifa kamili na kujiandaa kikamilifu kabla ya kutoa mimba.Hakikisha umesoma tena taarifa yote na una vitu vyote utakavyohitaji kabla ya muda, ikiwemo mpango wa usalama. Kukuwa na taarifa kamili kuna changia pakubwa kuwepo na utoaji mimba wa kimatibabu ulio salama.

1. Mimba kikokotoleo (calculator)
2. Vya Kuzingatia
3. Ushauri Wa Jumla
4. Kutengeneza mpango wa usalama
Pregnacy calculator

Mimba kikokotoleo (calculator)

Ujauzito wako ni wa muda gani? Utafiti unaonyesha kuwa mara nyingi utoaji mimba wa kimatibabu unapendekezwa zaidi kwa mimba zenye umri chini ya wiki 13 tangu hedhi yako ya mwisho. Tumia kikokotoleo (calculator) cha mimba ili kujua ujauzito una muda gani tangu hedhi yako ya mwisho.

Ikiwa hedhi yako ya mwisho ilianza tarehe au baadaye:

19 Septemba 2024

Bado unaweza kuzingatia kutumia tembe za kutoa mimba

Je mimba yako imepita wiki 13?

Taratibu ya HowToUseAbortionPill imekusudiwa kwa mimba zilizo hadi wiki 13. Hata hivyo, tembe za kutoa mimba zinaweza kutumiwa baadaye kwa mimba zenye umri zaidi kwa kufuata utaratibu mwingine.

Kwa taarifa zaidi, unaweza kuwasiliana na marafiki wetu kwenye www.womenonweb.org. Au enda kwenye ukurasa wa wasifu wa nchi ili kujifunza zaidi kuhusu rasilimali za utoaji mimba katika nchi yako.

Vya Kuzingatia kabla ya kutumia tembe za kutoa mimba

Ushauri Wa Jumla

iconKula kabla ya kutumia tembe. Ni bora kukuwa na chakula tumboni wakati unatoa mimba kwa kutumia tembe
iconKunywa maji mengi kipindi chote cha mchakato huu. Kukuwa na maji mwilini kutasaidia kupunguza maumivu.
iconWakati unatumia tembe za misoprostol,kuwa kwenye eneo (kama nyumbani mwako) ambapo una faragha na unaweza kujilaza na kupumzika kwa masaa machache baada ya kutumia dawa ikiwa utahitaji kupumzika.
iconNi bora kuwa na mtu karibu anayeweza kukusaidia wakati wa mchakato wa kutoa mimba.
iconInashauriwa kunywa tembe za ibuprofen kabla ya kuitumia misoprostol kusaidia kupunguza maumivu.
iconHakikisha umeweka tayari mpango wa usalama kabla ya kutumia tembe za kuavya mimba, hili ni la muhimu iwapo utahitaji msaada wa matibabu ya dharura.

Kutengeneza mpango wa usalama

Kulingana na Shirika la Afya Duniani (WHO) , uavyaji wa mimba kwa kutumia tembe ni salama na ni nadra matatizo yatokee. Hata hivyo, unapaswa kujitayarisha ipasavyo kwa matibabu ya dharura kama itahitajika. Zingatia maswali yetu hapa chini ili kusaidia kutengeneza mpango wako wa usalama iwapo utaihitaji.

Marejeo:

HowToUseAbortionPill.org inashirikiana na shirika lisilo la faida lililosajiliwa huko Amerika-501c (3)
HowToUseAbortionPill.org hutoa yaliyomo yaliyokusudiwa kwa sababu ya habari tu na haihusiani na shirika la matibabu.

    Inaendeshwa na Women First Digital