Masharti ya huduma

Kwa ujumla

Kwa kutumia Huduma, unakubali Sheria na Masharti yote kutumika kama tunavyoweza kusasishwa mara kwa mara. Unapaswa kusoma ukurasa huu mara kwa mara ili ujue mabadiliko yoyote ambayo tunaweza kuwa tumefanya kulingana Masharti ya Huduma.

Tuna haki ya kuondoa au kurekebisha Huduma bila taarifa. Haitakuwa makosa yetu ikiwa kwa sababu yoyote, Tovuti hii haipatikani wakati wowote na kwa muda wowote. Mara kwa mara, tunaweza kuzuia ufikiaji kwa sehemu zingine za Tovuti hii au kwa Tovuti yote.

Tovuti hii inaweza kuwa na viunganisho kuelekea tovuti zingine (“Tovuti Zilizounganishwa”), ambazo haziendeshwi na www.howtouseabortpill.org. Tovuti hii haina udhibiti wa Tovuti zilizounganishwa na haikubali jukumu lolote kwao au kwa upotezaji wowote au uharibifu unaoweza kutokea kutokana na matumizi yako. Matumizi yako ya Tovuti zilizounganishwa zitategemea masharti ya matumizi na huduma iliyomo ndani ya kila tovuti kama hiyo.

Sera Kuhusu Faragha

Sera yetu kuhusu faragha ambayo inaelezea jinsi tutatumia habari kukuhusu, inaweza kupatikana katika www.howtouseabortionpill.org/sw/privacy-policy. Kwa kutumia Tovuti hii, unakubali mfumo ulioelezewa ndani na unathibitisha kuwa data yote uliyotupa ni sahihi.

Makatazo

Haupaswi kutumia Tovuti hii vibaya. Hautaweza: kufanya au kuhimiza kosa la jinai; kupitisha au kusambaza virusi, trojan, minyoo, bomu ya mantiki au nyenzo nyingine yoyote ambayo ni mbaya, yenye madhara katika teknolojia, kwa kukiuka uhakika au kwa njia yoyote ya kukera au ya kuchukiza; kuingilia mawasiliano katika nyanja yoyote ya Huduma; data mbovu; kusababisha kero kwa watumiaji wengine; kukiuka haki za umiliki wa mtu mwingine yeyote; kutuma matangazo yoyote yasiyotakikana au nyenzo za uchochezi ambazo hujulikana kama “jumbe za kero”; au kujaribu kuathiri utendaji wa vifaa vyovyote vinvyohusiana na tarakilishi au kupatikana kupitia Tovuti hii.”

Kuvunja kifungu hiki itakuwa kosa na www.howtouseabortionpill.org itatoa ripoti kuhusu ukiukaji wowote kwa mamlaka husika za utekelezaji wa sheria na kukutambulisha kwa mamlaka hizo.

Halitakuwa kosa letu kwa upotezaji wowote au uharibifu unaosababishwa na shambulio la kukana huduma, virusi au vifaa vingine vyenye teknolojia ambavyo vinaweza kuambukiza vifaa vyako vya tarakilishi, programu za tarakilishi, data au vifaa vingine vyenye umiliki kwa sababu ya matumizi yako ya Tovuti hii, unapopakua nyenzo yoyote iliyochapishwa juu yake, au kwenye Tovuti yoyote iliyounganishwa na hii.

Mali za kitaaluma, Programu na Yaliyomo

Haki miliki zilizomo katika programu zote na yaliyomo (hii ikiwa ni pamoja na picha) ambayo yanapatikana kupitia Tovuti hii bado ni mali ya www.howtouseabortpill.org au watoa leseni zake na inalindwa na sheria na mikataba ya hakimiliki ulimwenguni kote. Haki zote hizo zimehifadhiwa na www.howtouseabortpill.org na watoa leseni zake. Unaweza kuhifadhi, kuchapisha na kuonyesha yaliyomo tu kwa matumizi yako ya kibinafsi. Hauruhusiwi kuchapisha, kuendesha, kusambaza au kutoa kwa muundo wowote, yaliyomo au nakala za yaliyomo uliyopewa au ambayo yanaonekana kwenye Tovuti hii wala huwezi kutumia mambo yoyote yaliyomo kuhusiana na biashara yoyote au kibiashara.

Kanusho la Dhima

Mambo yote yaliyomo na nyenzo zinazotolewa kwenye Tovuti zimekusudiwa kutoa habari ya jumla, majadiliano ya jumla, na elimu tu. Mambo yaliyomo hutolewa “kama ilivyo,” na matumizi yako au kutegemea kutumia vifaa kama hivyo ni hatari kwako mwenyewe.
Kwa hali yoyote, www.howtouseabortpill.org haitawajibika kwa upotezaji au uharibifu wowote, pamoja na jeraha la kibinafsi linalotokana na yale yaliyomo kwenye Tovuti au mwingiliano wowote kati ya watumiaji wa Tovuti, iwe ni mtandaoni au nje ya mtandao.

Kuunganisha na Tovuti hii

Unaweza kuunganisha na ukurasa wetu wa mwanzo ikiwa utafanya hivyo kwa njia ya haki na ya kisheria na isiyoharibu sifa yetu au kufaidika kutokana nayo, lakini haupaswi kuanzisha kiungishi kwa njia ya kupendekeza fomu yoyote ya ushirika, idhini au egemeo kwa upande wetu ambapo hakuna. Haupaswi kuanzisha kiunganishi kutoka kwa Tovuti yoyote ambayo hauimiliki. Tovuti hii haipaswi kuunganishwa na tovuti nyingine yoyote, na wala hauwezi kuunda kiunganishi kwa sehemu yoyote ya Tovuti hii isipokuwa ukurasa wa mwanzo. Tuna haki ya kuondoa ruhusa ya kuunganisha bila taarifa yoyote.

Kanusho kuhusu umiliki wa alama za biashara, picha za haiba na hakimiliki ya mtu mwingine
Isipokuwa pale ambapo imeelezwa waziwazi, lakini watu wote (ikiwa ni pamoja na majina na picha zao), alama za biashara za mtu wa tatu na yaliyomo, huduma na / au maeneo yaliyoonyeshwa kwenye Tovuti hayahusiani, kuunganishwa au kushirikishwa na www.howtouseabortpill.org. na haupaswi kutegemea uwepo wa unganisho au ushirika kama huo. Alama za biashara au majina yoyote yaliyoonyeshwa kwenye Tovuti hii yanamilikiwa na wamiliki wa alama za biashara husika. Ambapo alama ya biashara au jina la chapa limetajwa hutumika tu kuelezea au kutambua bidhaa na huduma na sio kusisitiza kwamba bidhaa au huduma hizo zinaidhinishwa na au zina uhusiano na www.howtouseabortpill.org.

Fidia

Unakubali kutoa fidia, kutetea na kutokubali kuharibiwa kwa www.howtouseabortpill.org, wakurugenzi wake, maafisa, wafanyikazi, washauri, mawakala, na washirika, kutoka kwa madai yoyote ya mtu mwingine, dhima, uharibifu na / au gharama (pamoja na ada ya kisheria) inayotokana na utumiaji wako wa Tovuti hii au ukiukaji wako wa Sheria na Masharti.

Mabadiliko

Wakati wowote na kwa hiari yake, www.howtouseabortpill.org itakuwa na haki na bila taarifa ya kurekebisha, kuondoa au kutofautisha Huduma na / au ukurasa wowote wa Tovuti hii.

Ubatilifu

Ikiwa sehemu yoyote ya Sheria na Masharti haiwezi kutekelezeka (pamoja na kifungu chochote ambamo hakuna dhima yetu kwako) utekelezaji wa sehemu nyingine yoyote ya Masharti ya Huduma haitaathiriwa. Vifungu vingine vyote vinabaki vikitumika kikamilifu. Kwa kadri inavyowezekana ambapo kifungu chochote / kifungu kidogo au sehemu ya kifungu / kifungu kidogo kinaweza kuwekwa kando na kuacha sehemu iliyobaki kuwa halali na kifungu hicho kitatafsiriwa ipasavyo. Vinginevyo, unakubali kwamba kifungu hicho kitarekebishwa na kutafsiriwa kwa njia ambayo inafanana kabisa na maana asili ya kifungu / kifungu kidogo kama inavyoruhusiwa kisheria.

Malalamiko

Tunatumia utaratibu wa kushughulikia malalamiko ambayo tutatumia kujaribu kutatua mizozo wakati inapoibuka kwanza, tafadhali tujulishe ikiwa una malalamiko au maoni yoyote.

Msamaha

Kama utakiuka masharti haya na hatuchukui hatua yoyote, bado tunastahili kutumia haki zetu na suluhu katika hali nyingine yoyote ambapo unakiuka masharti haya.

Mkataba Mzima

Masharti ya Huduma yaliopo hapo juu yanajumuisha makubaliano yote ya wahusika na yanachukua nafasi ya makubaliano yoyote yaliyotangulia na ya wakati wote kati yako na www.howtouseabortpill.org. Msamaha wowote unaohusiana na kifungu chochote cha Masharti ya Huduma utafanya kazi tu ikiwa kwa maandishi na kutiwa saini na Mkurugenzi wa www.howtouseabortpill.org.

HowToUseAbortionPill.org inashirikiana na shirika lisilo la faida lililosajiliwa huko Amerika-501c (3)
HowToUseAbortionPill.org hutoa yaliyomo yaliyokusudiwa kwa sababu ya habari tu na haihusiani na shirika la matibabu.

    Inaendeshwa na Women First Digital