Sisi Ni Nani & Kadiri Ya Sera Hii:

HowToUseAbortionPill (shirika ama Sisi) ni shirika lisilo la faida ambalo hutoa mfumo wa kidijitali wenye tovuti na teknolojia zinazohusiana ili kuwapa watu duniani kote taarifa sahihi na zilizowekwa maalum kuhusu tembe salama za uavyaji mimba, na kuwawezesha kutoa mimba kwa njia salama kwa masharti yao wenyewe (Mfumo).Mfumo huu hukusanya taarifa zinazoweza kumtambulisha mtu binafsi (PII) kuhusu watumiaji wake, ikiwa ni pamoja na wafanyakazi wa Shirika, wafanyakazi huru, na waombaji kazi (Watumiaji). Sera hii ya Faragha inaangazia aina za PII tunazokusanya na haki za Watumiaji kuhusu PII zao. Ingawa tunadhibiti vipengele vingi vya Mfumo, vipengele fulani hutolewa na Watoa Huduma wa Nje ili kuimarisha ufanisi wake.
Sera hii ya Faragha ilianzishwa ili kulinda faragha ya Watumiaji.

Mabadiliko Kwa Sera Hii Na Ilani Za Ziada Za Faragha

Tunadumisha haki ya Kubadilisha Sera hii ya Faragha katika siku zijazo. Hatutawajulisha watumiaji kuhusu mabadiliko madogo ambayo hayaathiri faragha yao kwa kiasi kikubwa – kama vile kutoa ulinzi wa faragha ulioboreshwa, kurekebisha hitilafu za uchapaji au kuongeza maelezo ya ziada. Kwa mabadiliko yoyote makubwa, tutawajulisha Watumiaji kupitia barua pepe. Bila anwani halali ya barua pepe kutoka kwa Mtumiaji, hatuwezi kumfahamisha kuhusu mabadiliko yoyote ya Sera. Sera hii ya Faragha inaweza kusasishwa au kuongezwa nasi kupitia matoleo mapya au arifa za ziada za faragha zinazohusiana na mwingiliano mahususi nasi. Arifa hizi zinaweza kuongezwa katika Sera hii, kuchapishwa kwenye tovuti ya Shirika, na/au kupatikana kwako kivyake.

Viungo Kwa Tovuti Zingine

Sera hii ya Faragha haiendelei hadi tovuti za watu wengine ambazo zinaweza kuunganishwa au kufikiwa kutoka kwa Mfumo. Hatuwajibiki kwa maudhui, vipengele, utendakazi, au desturi za faragha za tovuti au huduma kama hizo zilizounganishwa. Ukusanyaji wa data na matumizi ya tovuti yoyote iliyounganishwa ya wahusika wengine inasimamiwa na notisi, taarifa au sera ya ya faragha zao. Tunakuhimiza uzisome.

Taarifa Zilizokusanywa Zinazoweza Kumtambulisha Mtu Binafsi:

Katika Sera hii ya Faragha, maelezo yote yanayoweza kumtambulisha mtu binafsi kwa pamoja yanaitwa “PII.” Tunakusanya anuwai mpana wa PII kutoka kwa na kuhusu Watumiaji, kulingana na Mtumiaji na muktadha. Kwa hivyo, PII inaweza kujumuisha:

  • Jina.
  • Anwani ya barua pepe.
  • Nambari ya simu.
  • Anwani ya IP, mtoa huduma wa intaneti, aina ya kivinjari na lugha.
  • Eneo.
  • Majira ya Saa.
  • Lugha zilizotumika.
  • Umri, jinsia, picha za kibinafsi na taarifa zingine za kibinafsi ambazo Watumiaji hutoa.
  • Taarifa Watumiaji hutoa kuhusu afya zao, masuala ya uzazi/mimba, sababu za kuingia katika Mfumo, na uwezo wao wa kufikia na kulipia huduma za afya ya uzazi.
  • Hali ya ajira na taarifa kuhusu mwajiri.
  • Ushuhuda na ukadiriaji unaotolewa kwa kipengele chochote cha Mfumo.

Ukusanyaji Wa Taarifa Zako Za Kibinafsi:
Tunaomba idhini kabla ya kukusanya PII. Kwa kuingia katika Mfumo, Watumiaji wanakubali (1) sheria na masharti ya Sera hii ya Faragha na (2) ukusanyaji, utumiaji na uhifadhi wa maelezo wanayotoa na kwamba Mfumo ukusanye kutokana na matumizi yao ya teknolojia.
Kwa maneno mengine, wakati wowote Mtumiaji anapoingia katika Mfumo, inaweza kukusanya PII kiotomatiki kutoka kwa teknolojia ambayo Mtumiaji anatumia na itakusanya PII yoyote ambayo Mtumiaji hutoa wakati anapoingia katika Mfumo.

Mbinu za Ukusanyaji wa Taarifa za Kibinafsi:

  • Michango ya hiari ya Watumiaji;
  • Maingiliano ya watumiaji katika Mfumo, ikiwa ni pamoja na Watoa Huduma wa Nje/Wahusika Wengine.
  • Mazungumzo na Watumiaji.

Tunaendelea kutafuta mbinu bora na salama za ukusanyaji wa PII, na tutasasisha Sera hii ya Faragha ili kuonyesha mbinu mpya.

Jinsi Tunavyotumia Maelezo Yako Binafsi:

Tunatumia PII tunayokusanya na/au kumiliki kwa njia zifuatazo:

  • Kutangamana nawe kama Mtumiaji ikijumuisha, kati ya mengine, kukupa taarifa zinazofaa na muhimu ambazo zinahusiana na chaguo zako za uzazi.
  • Kuchanganua PII yoyote ili tuweze kuboresha huduma, bidhaa na thamani tunayotoa na/au kuwasiliana kuhusu maboresho kama haya na taarifa zinazohusiana kwa Watumiaji na watu wengine.
  • Kutekeleza kazi za usimamizi za Mfumo na/au katika hali ya kawaida ya ajira na uendeshaji wa Shirika.
  • Kufanya utafiti ya na/au na Shirika.
  • Kwa baadhi ya kozi za mtandaoni tunazotoa kwa ushirikiano na mashirika mengine, tunayapa mashirika hayo mengine baadhi ya PII tunayokusanya kuhusu wanachama wao wanaoshiriki katika kozi kama hizo za mtandaoni.
  • Kwa juhudi za kuchangisha pesa, ambazo zinaweza kujumuisha kutoa muhtasari wa PII kwa mashirika yanayotoa au yanoweza kutoa ufadhili kwa Shirika.
  • Kutoa PII kwa watekelezaji sheria, mashirika au mamlaka mengine ya serikali, au wahusika wengine kama inavyotakiwa na sheria inayotumika, amri ya mahakama, wito wa mahakama au mchakato wa kisheria unaotolewa kwa Shirika.

Tutachukua hatua za busara na halali ili kuepuka kulazimishwa kufichua PII yako na shirika lolote la kiserikali au wahusika wengine ambao wanataka kuifikia. Hata hivyo, kuna matukio ambapo shirika za serikali na/au wahusika wengine wana haki ya kisheria ya kushurutisha mashirika kama vile Shirika letu kufichua PII; na, katika hali hizi, Shirika letu litalazimika kutii.
Kuhusu PII iliyokusanywa na/au kuhifadhiwa na Watoa Huduma Wengine wanaoshiriki katika Mfumo, hatudhibiti matumizi yao na/au uhifadhi wa PII yoyote kama hiyo.
Kama ilivyofafanuliwa katika sehemu ya Sera ya Faragha inayoitwa “HAKI ZAKO JUU YA TAARIFA ZAKO ZA KIBINAFSI”, unaweza kushawishi tunachofanya na PII yako kama ilivyofafanuliwa katika sehemu hiyo.

Haki Zako Juu Ya Taarifa Zako Za Kibinafsi:

Haki za watumiaji kuhusu PII yao zinajumuisha:

  • Kufikia na kupokea nakala za PII yao.
  • Kuelewa jinsi PII yao imepatikana na kutumika.
  • Kusahihisha au kufuta PII yao.
  • Kubadilisha jinsi tunavyotumia PII yao.

Ili kutekeleza mojawapo ya haki hizi, ni lazima Watumiaji watupe barua pepe halali, inayoweza kuthibitishwa na wafuate maagizo yaliyowekwa hapa chini katika sehemu ya Sera hii ya Faragha yenye kichwa “JINSI YA KUWASILIANA NASI KWA MAOMBI, MAONI NA MASWALI”. Ikiwa Mtumiaji hatatupa barua pepe halali, inayoweza kuthibitishwa, hatuwezi kuwasiliana naye; na hii inatuzuia (1) tusimfahamishe kuhusu mabadiliko kwenye sera hii na/au masuala yanayohusiana na PII yao (2) na sisi kuthibitisha utambulisho wao ili tuweze kuwaruhusu kutumia haki zao za kufikia, kusahihisha, kudhibiti na kufuta PII yao.

Sera Ya Faragha Na Mazoea Ya Shirika Kuhusu Watoto:

Hatusanyi data kimakusudi kutoka kwa watu walio na umri wa chini ya miaka 13. Kwa kuwa Mfumo wetu haulengi watoto, hatuthibitishi umri wa watumiaji wanaotumia tovuti na huduma zetu. Hii inamaanisha kuwa tunaweza kukusanya bila kukusudia na bila kujua baadhi ya PII ya mtoto anayetumia Mfumo. Kwa kiwango ambacho Watumiaji watatoa PII kuhusu watu walio na umri wa chini ya miaka 13, Shirika litashughulikia PII kama hiyo kulingana na Sera hii ya Faragha. Ikiwa tutatangamana na mtu na tujue kwamba ana umri wa chini ya miaka 13, tutamwagiza mtu huyo kwamba anahitaji kibali cha mzazi ili atumie Mfumo.

Usalama Wa Data Na Sera Na Mazoea Ya Uhifadhi:

Ili kulinda PII yako, tunachukua hatua zifuatazo:

  • Elimu kuhusu Sera hii: Tunawaelimisha wafanyakazi wetu, washirika, na Watoa Huduma Wengine kuhusu maelezo ya Sera hii ya Faragha, tukisisitiza jukumu muhimu wanalochukua katika kuzuia ufikiaji au matumizi yasiyoidhinishwa ya PII chini ya ulinzi wao.
  • Uimarishaji wa Usalama: Ahadi yetu inayoendelea ya kuimarisha usalama wa PII inaonekana katika juhudi zetu za sasa. Tayari tumeweka itifaki kadhaa za usalama zinazolenga kuzuia ufikiaji au matumizi mabaya ya PII ambayo hayajaidhinishwa. Baada ya kukamilisha mipango yetu ya kuboresha usalama, tutatoa muhtasari uliyosasishwa wa hatua hizi katika Sera hii ya Faragha. Jisikie huru kuwasiliana nasi kwa ufafanuzi wowote.
  • Sera ya uhifadhi wa data: Kwa kawaida, utaratibu wetu ni kufuta PII zote mwaka mmoja baada ya upataji wake. Walakini, kwa kuzingatia upana wa Mfumo wetu, hatuwezi kufaulu kufuata ratiba huu wa muda kila mara. Ni muhimu kukumbuka kwamba sera hii ya uhifadhi haitumiki kwa PII iliyokusanywa au kuhifadhiwa na Watoa Huduma Wengine.
  • Sera ya usimbaji fiche wa data: Kwa kutambua umuhimu wa usimbaji fiche wa PII iliyokusanywa, tunabadilisha Mfumo wetu ili kuhakikisha usimbaji fiche kamili wa PII. Kwa sasa, mchakato huu haujatekelezwa kikamilifu katika PII yote. Zaidi ya hayo, mkakati huu wa usimbaji fiche haujumuishi PII chini ya ulinzi wa Watoa Huduma Wengine.
  • Watoa Huduma Wengine: Kuhusu Watoa Huduma Wengine, hatujafanya uthibitishaji huru wa hatua zao wanazodai za usalama. Tathmini kama hiyo huru ni ghali sana na inachukua muda kwa shirika kama Shirika letu; na watoa huduma wengine wengi hawataruhusu tathmini hizi kufanywa.

Ufichuzi Wa “USIFUATILIE”

Hatufuatilii watu kwenye tovuti za wahusika wengine ili kutoa utangazaji unaowalenga. Kwa hivyo, hatujibu mawimbi ya Usifuatilie (DNT).

Jinsi Ya Kuwasiliana Nasi Kwa Maombi, Maoni, Na Maswali:

Kwa maombi, maoni au maswali, tutumie barua pepe kwenye info@howtouseabortionpill.org. Tunathibitisha vitambulisho kwa kutumia barua pepe iliyo kwenye faili kabla ya kujadili PII.
Kama ilivyoelezwa hapo juu, ikiwa Mtumiaji hatatupa barua pepe halali, inayoweza kuthibitishwa wakati anawasiliana nasi mara ya kwanza na kutupatia PII, hatuwezi kuthibitisha utambulisho wake; na hii inatuzuia kuruhusu mtu yeyote kutumia haki zozote zinazohusiana na PII tunayomiliki.

Sasisho La Mwisho:

Sera hii ya Faragha ilisasishwa tarehe 1 Januari 2025. Tutasasisha Sera hii ya Faragha angalau mara moja kila baada ya miezi 12.