Namna Tembe ya utoaji mimba kimatibabu Inavyofanya kazi
Mifepristone huzuia mimba kuendelea kukuwa, na husaidia kufungua shingo ya mfuko wa kizazi (eneo la kuingia mji wa mimba).Misoprostol husababisha mji wa mimba kukaza na hatimaye kusukuma mimba nje.
Mara misoprostol imenyonywa mwilini, utaanza kuumwa tumbo na kutokwa damu.Kwa kawaida hii itaanza ndani ya saa 1 hadi 2 baada ya kumeza dawa za kwanza. Kwa kawaida, mimba hutoka ndani ya saa 24 baada ya kumeza dawa za mwisho za misoprostol.Mara nyingi, itafanyika kabla ya hapo.
Una wasiwasi baada ya kutumia tembe za utoaji mimba?
Hapa chini kuna njia kadhaa za kutambua ikiwa utoaji mimba umefaulu:
- Unaweza kutambua vijinyama vya mimba (tishu) wakati vinatoka. Vinaweza kufanana na damu iliyoganda yenye rangi nyeusi na ina utando mwembamba, au kama kifuko kidogo kilichozungukwa na utando mlaini mweupe. Kulingana na umri wa mimba, tishu hii inaweza kuwa ndogo kuliko ukucha wako, au hadi kufikia ukubwa wa kidole gumba.
- Kutokwa damu wakati wa mchakato wa kutoa mimba ni sawa na kutokwa damu wakati wa hedhi, au damu inaweza kuwa nyingi zaidi.
- Dalili zako za mimba zitapungua.Vitu kama maumivu ya matiti, kichefuchefu, na uchovu vitaanza kupungua.
Marejeo:
- “Induced Abortion.” American College of Obstetrics and Gynecologists.
https://www.acog.org/Patients/FAQs/Induced-Abortion - “Care for Women Choosing Medication Abortion.” The Nurse Practitioner.
https://journals.lww.com/tnpj/Citation/2004/10000/Care_for_Women_Choosing_Medication_Abortion.9.aspx - “Safe abortion: technical and policy guidance for health systems.”The World Health Organization.
https://apps.who.int/iris/bitstream/handle/10665/70914/?sequence=1