Utoaji mimba kwa kujitegemea
Masomo haya ya mtandaoni yanalenga mtu yeyote anayetaka kujifunza zaidi kuhusu utoaji-mimba yeye mwenyewe, au kutoleya mimba nyumbani. Unapokuwa na habari ambayo utapata katika masomo haya, unaweza saidia kuhakikisha kuwa utoaji mimba kwa kutumia vidonge ni salama na vinapatikana. Masomo haya yanatolewa kwa ushirikiano wa Madaktari Wasio na Mipaka (Médecins Sans Frontières) na www.HowToUseAbortionPill.org
Somo la 1. Nina ujauzito?
Ungependa kuwa na uhakika kuhusu ya ujauzito wako? Pitia-pitia katika video hii kwa habari zinayohusiana na uthibitisho wa ujauzito
Ujauzito, Kupata ujauzito
Ujauzito – uliyopangwa na usiyopangwa – ni uzoefu wa kawaida sana.
Ulimwenguni kote, zaidi ya 40% ya ujauzito kote ni yule haujapangwa.
Ikiwa haukutaka kupata ujauzito lakini unafikiria kuwa unaweza kuwa nao, si wewe peke yako.
Katika video hii, tutazungumzia jinsi ya kudhibitisha ujauzito.
Kwanza, ni muhimu kujua kwamba ujauzito hutokea baada ya kufanya mapenzi wakati shahawa inapotoka katika uume na kwenda ndani ya uke.
Dawa ya kuzuia mimba husaidia kuzuia ujauzito wakati wa ngono, lakini bado kuna uwezekano mdogo ambapo waweza kujipata mjamzito.
Ishara ya mwanzo na ya kuaminika ya ujauzito ni kukosa kipindi cha hedhi.
Ikiwa umefanya mapenzi na kugundua kuwa damu yako ya kila mwezi imechelewa, inawezekana kuwa wewe ni mjamzito.
Ishara zingine za kawaida za ujauzito ni pamoja na kichefuchefu, maumivu ya kichwa, kuhisi uchovu, kunenepa na kuwa na matiti laini.
Ikiwa una dalili hizi, pamoja na kukosa kipindi cha hedhi, kuna uwezekano kwamba wewe ni mjamzito.
Ikiwa unafikiria unaweza kuwa wewe ni mjamzito, unaweza kuthibitisha hili kwa kuchukua vipimo wa ujauzito ukitumia mkojo.
Kwa kawaida, vipimo vya ujauzito hupatikana katika maduka ya dawa na maduka madogo, au unaweza kwenda kwa kituo cha huduma za afya na kupata.
Si sharti kuchukua vipimo wa ujauzito kabla ya kutoa mimba kwa kutumia vidonge.
Ikiwa una dalili za ujauzito, au ikiwa imethibitika kuwa una ujauzito na hautaki kuwa mjamzito, unaweza amua kumaliza ujauzito.
Utoaji mimba unaweza ukafanyika kwa kutumia vidonge au kupitia njia ya upasuaji.
Tunapotoa habari za kweli, fuata mfululizo huu wa video ambayo inayotegemea uthibitisho na kujibu maswali yanayoulizwa mara nyingi kuhusu utoaji mimba kwa kutumia vidonge kabla ya wiki 13.
Katika video yetu inayofuata, tunajibu swali kama, *”Je! Muda wa ujauzito wangu umeenda umbali gani?*””
“